TATIZO KATIKA PRINTA YA EPSON
Si ajabu kwa watu wanaotumia printa aina ya epson kukutana na tatizo hili baada ya kutumia printa yake kwa muda fulani. Kuna kipindi nilihitaji kununua printa kwa ajili ya kufanyia shughuli ya biashara ya kutoa copy, kuprinti document na kusafisha picha. Niliombaushauri kwa mtu ambaye ni mzoefu katika shughuli hii, baada ya kuongea naye alinishauri ni nunue printa aina ya epson, ambayo inauwezo wa kuscan, kuprinti na kutoa kopi lakini alinishauri isingekua vizuri kutumia printa hiyo kutoa kopi za kawaida na kuprinti picha kwa sababu nikifanya hivyo upelekea printa hii kufa baada ya muda mfupi. Baada ya kufuatilia nimegundua si kweli inakufa bali inawahi kukumbwa na tatizo hili. Kwa nini nasema hivyo, kwa sababu ukiwa unafanya biashara ya kusafisha picha na kutoa kopi utakuja kugundua unapatawateja wengi zaidi wa kutoa kopi kuliko kusafisha picha. hii upelekea printa yako kuwahi kupatwa na tatizo h...